falling love

mmmmh


oo

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Tuesday, May 19, 2015

mkasa

Mwanzoni sikumpenda kutoka moyoni, nilimpenda kwa kuwa tu alikuwa mrembo haswa..kwa kifupi nilimtamani tu….yaani nilitegemea akinivulia nguo zake tukashiriki tendo hamu yangu itaisha na nitaachana naye. Ndio ningeachana naye kwa sababusikuona umuhimu wa kudumu na msichana ambaye sijui hata kama nitamuoa. Nilipomwambia tutaoana hakika nilidanganya Alinipenda sana, kadri siku zilivyokwenda alizidisha upendo wake kwangu. Hakuna nilichohitaji kwake akaninyima, aliwahi kumdanganya baba yake kuwa anaumwa akatumiwa pesa ilimradi anipatie mimi nilipomwambia kuwa kuna mtu ananidai na abananisumbua kwelikweli. Alisikitika kusikia vile, akaahidi kunipigania. Haikuwa kweli nilichomwambia juu ya kudaiwa, pesa ile aliyonipa niliitumia kulipia chumba nikafanya uzinzi na Fatuma. Alihadithiwa habari hiyo na marafiki walioniona nikiingia kule, akalia kwa uchungu mbele yangu, lakini neno lake la mwisho likabaki kuwa ‘NAKUPENDA SANA…..WEWE NI MWANAUME WA MAISHA YANGU’……..Nilij isikia vibaya lakini nafsi nyingine ikanikumbusha kuwa nilikuwa katika mahusiano na msichana yule kwa sababu moja tu…NGONO… na katu hakutaka kushiriki ngono na mimi. Alinikwepa sana hadi nikajisikia vibaya. Nikahisi huenda ana mtu mwingine. Hakika nilidhani kuwa anajihusisha na mtu mwingine ambaye hushiriki naye tendo hilo la ngono ambalo kwangu mimi kilikuwa kitu pekee ambacho kingeweza kuniaminisha kuwa ananipenda kweli. Msichana mrembo kama huyo kamwe asingeweza kuishi bila kufanya mapenzi. Hakika haikuniingia akilini. Wangapi wenye ,ali zao wanamtongoza, yeye ni nani hadi asiingie majaribuni?? Hapana ni uongo mtupu ananiongopea mimi. Nikaendelea na vimbwanga vya hapa na pale. Hakuchoka kunibembeleza, hakuchoka kunipenda na hakuchoka kunikumbusha kuwa ni mimi pekee nilikuwa katika moyo wake wa nyama. “Nikipotea jumla nd’o utajua kuwa nilikuwa nakupenda..” aliwahi kunambia neno hilo. Japo lilinigusa lakini sikulitilia maanani. Hatimaye tukamaliza shule, nikategemea kuwa ule muda wa kumfaidi msichana yule kingono ulikuwa umewadia. Lakini haikuwa hivyo, akaendelea kuwa mgumu huku akijitetea kwa sababu zisizokuwa na kichwa wala miguu. Mwanzoni nilidhani kuwa aliogopa kufanya mapenzi kabla hajamaliza shule, lakini ajabu hadi tulipomaliza bado alisimamia msimamo. Sasa nikajikuta katika pepo mbaya, nikaanza kumwonyesha hadharani kuwa nina wanawake wengine. Japo chozi lake liliniumiza sana lakini sikujali. Kwa nini ananinyima penzi binti huyu? Nilijiuliza. Hatimaye nikafikia uamuzi wa kuachana naye. Lakini siwezi kuachana naye bila kumjua ladha yake. Nilijiapia kuwa jambo hilo haliwezekani hata kidogo, mimi kama mwanaume kamili atanitangazaje kwa marafiki zke, kuwa sijawahi kulala naye tukafanya tendo??? Aibu kubwa!!! Nikampangia shambulizi moja la mwisho na kama ni ubaya uwe ubaya tu. Ilimradi nilishapanga kuachana naye….haitanidh uru lakini lazima nifanye naye tendo Nilimuita nyumbani kwangu, ilikuwa mida ya jioni. Alipofika nilimlaghai hapa na pale nikamgusa matiti yake madogo yaliyosimama wima yakijitahidi kunidhihaki. Na yalifanikiwa hasa hasa kunikebehi. Nikamgusa huku na kule..nilipotak a kumvua nguo akanizuia. Nilikuwa nimekunywa pombe kiasi hivyo sikuwa na aibu, nikaamua kutumia nguvu, niliamua KUMBAKA…..nikai chana sidiria yake, kisha nikaiondoa chupi yake sasa akabaki yu uchi wa mnyama. Alihaha huku na kule asiamini kile kinachotokea mbele yake. Nikamrukia ili niweze kutimiza lengo… Kamwe sikuwahi kumwona binti huyu akiwa katika uoga namna ile…alikuwa amekodoa macho yake….na alikuwa anatetemeka… Akataka kukimbia uchi, nikamdaka mkono nikamvutia pale nilipokuwa. Sikuwa nahuruma hata kidogo, nilichotaka ni itu kimoja tu..NGONO KISHA AKINICHUKIA NA ACHUKIE. Mara akatokwa na kelele kubwa sana zilizonishtua sana. Amakweli sikuzitegemea. Sikudhani kama amnaweza kufanya tendo lile “ANANIBAKAAAAA, NISAIDIEENI ANANIBAAAKA…..” ilikuwa kelele kubwa haswa, na alifanya kwa kurudia rudia Kelele zikawafikia wasamalia wema, binti akaendelea kupiga kelele. Hatimaye mlango ukavunjwa, wasamaria wakanivagaa na kuanza kunipiga……nilip igwa hadi nikapoteza fahamu. Nilipozinduka nilijikuta na pingu mkononi, pingu iliyounganishwa na kitanda. Nilikuwa na maumivu makali mwili mzima. Nikakumbuka kuwa nilifumaniwa nikitaka kufanya ubakaji. Pombe zilikuwa zimenitoka na niliona aibu wa kitendo cha kinyama nilichotaka kumfanyia Maria. Baada ya kujitambua vyema na nguvu kunrejea mwilini nilirejeshwa mahabusu. Nikaingia mahabusu nikikabiliwa na kesi mbaya ya ubakaji. SIKU NNE baadaye nilikuja kutolewa……hapak uwa na dhamana lakini ilikuwa barua tu ya kustaajabisha niliyokutana nayo. “Mpenzi Christopher mwanaume wa maisha yangu…..haikuwa nia yangu kukusababishia kipigo kikali na kuitwa mbakaji… nimefan ya haya kwa sababu nakupenda kutoka moyoni…napenda uishi miaka mingi..Chriss ni wewe mwanaume pekee niliyetokea kuvutiwa naye kihisia ukauteka moyo wangu na kujikuta nikiwa mtumwa wa mahaba yako… lakini nina mapungufu makubwa…nina kasoro kubwa ambayo hainipi hadhi ya kulala kitanda kimoja na wewe…..Chriss mimi ningekuwa muuaji iwapo ningekuruhusu unibake….hivi chriss unadhani mpapaso wako haukunisisimua? Nilisisimka haswa na nilitamani nikutimizie kwa hiari kile ulichotaka, labda mimi nilikuwa muhitaji kuliko wewe mpenzi lakini…..lakini nisingeweza kukuua, ….Chriss ninayo furaha na wala usisikitike kusikia hili, mimi nimefurahi sana kufa nikiupigania uhai wa mwanaume niliyempenda, ninayempenda na ninayekufa kwa ajili yake. Kitanzi hiki kiwe kumbukumbu yako milele kuwa NILIKUPENDA…….C hriss mimi ni muathirika wa gonjwa la UKIMWI niliambukizwa na wazzi wangu …nilizaliwa nikiwa na Ukimwi Chriss, mama kabla ya kufa alinikanya kuwa nisiwe na tabia kama ya marehemu baba ambaye alimuambukiza maksudi kutokana na taba yake ya kutotulia nyumbani, mama akanikanya kuwa ni heri nife peke yangu kuliko kuua yeyote asiyekuwa na hatia. Na huyo mtu ni wewe Chriss haukuwa na hatia na haukustahili kufa..…..laiti kama ungenibaka basi leo hii ningekufa nikiwa MUUAJI… ninafura hi kuwa nakufa kama SHUJAA. Nimeyaadika haya huku kitanzi kikiwa shingoni mwangu, nakufa leo lakini wakuache wewe huru. Huru kabisa, naenda kuungana na mama yangu nimweleze kuwa sikuwahi kuua duniani na nimeamua kuondoka ili siku moja nisije kuua yeyote. Ubaki salama Chris wangu” Nilijikuta napoteza fahamu tena baada ya kuhakikishiwa kuwa Maria alizikwa baada ya kujinyonga katika chumba chake nyumbani kwao nabaruaile ilikutwa chini ya miguu yake iliyokuwa unaning’inia……. nilipozinduka nilikuwa nyumbani kwetu…kila jicho lilinitazama kwa namna yake……wengine kwa hasira wengine dharau na baadhi kwa huzuni. AMA KWA HAKIKA nilikuwa na mpenzi aliyenipenda kwa dhati……. UPUMZIKE PEMA PEPONI Maria…..kamwe sitakusahau mpenzi……. UJUMBE; Usilipize baya kwa baya kwa kizazi kisichokuwa na hatia…..JIFUNZE kupenda kwa dhati lakini HISIA ZAKO ZISIKUFANYE MTUMWA!!!!
Read More ->>

ndoto

Kuna siku nilikuwa maeneo ya Mjini kati (City Center), nikaipenda suruali moja ya shilingi 15,000/= na pesa sikuwa nayo ikabidi niende kutoa kwenye ATM ya Postal. 
Nimefika pale sikukuta mtu hivyo niliingia moja kwa moja, nimefika mle ndani nikakuta Pesa Kibao zimemwagika pale kwenye kitundu cha kutolea pesa, ATM Card ilikuwepo pale imetokezea na Pembeni kulikuwa na Pochi ya Kike iliyoonekana kutuna vilivyo. 

Kwa woga mimi huku nikitetemeka mapigo ya moyo yakiwa yameongezeka nikatizama nyuma yangu sikuona mtu, nikachukua zile Pesa harakaharaka, ATM na ile pochi.
 
Ile natoka nje kuna dada mmoja alikuwa anakuja kwa kasi maeneo yale nikapata uoga nikamuuliza “Samahani dada, kuna kitu umesahau humu”, yule dada hakunijibu kitu kaingia kwenye chumba cha ATM akachomeka Kadi kutoa hela mi nikaondoka zangu fasta kuelekea home.
 
Nimefika home nikajifungia ndani na kuzibwaga zile pesa kitandani, nikafungua wallet nikakuta imejaa dollar, Vipodozi, iphone na ki-Nokia kidogo cha tochi, ATM Card mbili za Benki tofauti ambazo zilikuwa zimezungushiwa karatasi iliyokuwa na namba za siri za ATM zote, moyo ukanilipuka paaaa!!! Nikaona bora Nipumzike kwanza kitandani!!
 
Muda si mrefu ile iphone ikaanza kuita, nilipoangalia halikutokea jina nikaona bora nipokee nimsikilize anasemaje, ilikuwa sauti ya kike iliyoongea kwa huzuni kwa kubembeleza huku akilia na alijitambulisha vizuri kuwa ile mali ni ya kwake! Huruma ilinijia nikamwelekeza nilipo aje kuchukua...
 
Hakuchukua muda akawa amefika nami nikamkabidhi vitu vyote naye akavihakiki na kukuta viko sana: Milioni 3 za Kibongo na Dollar 500. Dada kanishukuru na kunipa ile Millioni 3 ya kibongo mi nikazikataa kwasababu ni mali yake na alizisahau tu.
 
Alinitoa hofu kwa kunisihi nichukue tu, mi kama binadamu mwenyezi Mungu atanilipa, nikakataa... Mwishowe akaomba namba yangu na kuondoka zake, akawa ameniacha ndani huku njaa sasa nikaanza kuisikia, nilikuwa na buku mbili nikaenda kula viepe kavu na soda nikawa powa.
 
Sasa jana kanipigia simu kuwa anakuja nimsubiri, dakika tano tu akanipigia tena kuwa ameshafika yupo nje yupo ndani ya Prado mpyaa nikaingia tukaondoka akaenda kunionyesha kwake kisha tukaelekea kwenye nyumba nyingine iliyokuwa ndo imekamilika kujengwa akaniambia hii itakuwa yako akanikabidhi baadhi ya nyaraka na funguo zote sikuamini...!!
 
Akanisindikiza kwangu, kufika home ananiambia hiyo gari (Prado) nayo ananiachia ni kwa mema tu niliyomfanyia, ndani ya ile gari kulikuwa na brifcase iliyokuwa na pesa akaniambia pia hii pesa itakuwa yako ya kuanzia maisha, na kumbe yule dada alikuwa kanipenda akanikumbatia kwa nguvu nikiwa pale kwenye seat oooh!! umasikini baibai...
 
Akiwa kanikumbatia akihema kwa kasi juu ya kifua changu nikahisi mtu akinishika begani na  kuniita kwa sauti.
“Anko ankoo we ankoo... amka rafiki yako Salim anakuita!!!”.
 
“ALIKUWA MTOTO WA SISTA ALIKUWA ANANIAMSHA !!”.
Kumbe muda wote nilikuwa nikiota Dah...!!
Read More ->>

visitors comments